Misaada ya Kujifunza
Eliya


Eliya

Nabii katika Agano la Kale ambaye alirudi katika siku za mwisho kuwatunukia funguo za uwezo wa kufunga Joseph Smith na Oliver Cowdery. Katika siku zake, Eliya alihudumu katika Ufalme wa Kaskazini wa Israeli (1 Fal. 17–22; 2 Fal. 1–2). Alikuwa na imani kuu katika Bwana na anajulikana kwa ajili ya miujiza mingi. Kutokana na maombi yake, Mungu aliizuia mvua kwa miaka mitatu 3½. Alimfufua mvulana kutoka kwa wafu na aliita moto kutoka mbinguni (1 Fal. 17–18). Watu wa Uyahudi bado wanasubiri kuja kwa Eliya, kama Malaki alivyotoa unabii kuwa angekuja (Mal. 4:5). Yeye anabakia mgeni mwalikwa katika Karamu ya Pasaka ya Kiyahudi, ambapo mlango ulio wazi na kiti kikiwa wazi daima vikimsubiri yeye.

Joseph Smith Nabii alisema kwamba Eliya alishikilia nguvu za kufunga za ukuhani wa Melkizedeki na alikuwa nabii wa mwisho kufanya hivyo kabla ya wakati wa Yesu Kristo. Yeye alionekana juu ya Mlima wa Kugeuka Sura pamoja na Musa na wakaweka funguo za ukuhani huo juu ya Petro, Yakobo, na Yohana (Mt. 17:3). Alionekana tena pamoja na Musa na wengine mnamo 3 Aprili 1836, katika Hekalu la Kirtland Ohio na akatunukia funguo hizo hizo juu ya Joseph Smith na Oliver Cowdery (M&M 110:13–16). Hii yote ilikuwa katika maandalizi kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana, kama ilivyonenwa katika Malaki 4:5–6.

Uwezo wa Eliya ni uwezo wa kufunga wa ukuhani ambao kwa huo mambo ambayo yanafungwa au kufunguliwa duniani hufungwa au kufunguliwa mbinguni (M&M 128:8–18). Watumishi wateule wa Bwana walio duniani leo wanao uwezo huu wa kufunga na kufanya ibada za injili zenye kuokoa kwa ajili ya walio wazima na wafu (M&M 128:8).