Katika maandiko, jicho daima limetumika kama ishara ya uwezo wa mtu kupokea nuru ya Mungu. Kama ishara, jicho la mtu pia huonyesha hali ya kiroho na uelewa wa mambo ya Mungu.
Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, 2Â Ne. 15:21 (Isa. 5:21 ).
Walianza kufunga na kusali ili macho ya watu yapate kufunguliwa, Mos. 27:22 .
Shetani aliyapofusha macho yao, 3Â Ne. 2:2 .
Hakuna anayeweza kuwa na uwezo wa kukitoa Kitabu cha Mormoni isipokuwa kwa jicho kuwa tu kwa utukufu wa Mungu, Morm. 8:15 .
Kwa uwezo wa Roho macho yetu yakafunguliwa na ufahamu wetu ukaangazwa, M&M 76:12 .
Nuru hutoka kwake yeye aangazaye macho yako, M&M 88:11 .
Kama jicho lako likiwa katika utukufu wangu, mwili wako wote utajawa na nuru, M&M 88:67 .