Wana na Mabinti za Mungu Ona pia Lipia dhambi, Upatanisho; Mwanadamu, Wanadamu; Watoto wa Kristo; Zaliwa; Zaliwa na Mungu, Zaliwa Tena Maandiko hutumia maneno haya katika njia mbili. Katika maana moja, sisi wote ni watoto halisi wa kiroho wa Baba wa Mbinguni. Katika maana nyingine, wana na mabinti za Mungu ni wale waliozaliwa tena kwa njia ya Upatanisho wa Kristo. Watoto wa kiroho wa Baba Ninyi ndinyi miungu, watoto wa Aliye Juu Sana, Zab. 82:6. Sisi wazao wa Mungu, Mdo. 17:29. Tujitie chini ya Baba wa roho, Ebr. 12:9. Mimi ni mwana wa Mungu, Musa 1:13. Watoto waliozaliwa tena kupitia Upatanisho Kadiri wengi walivyompokea aliwapa uwezo wa kuwa wana wa Mungu, Yn. 1:12 (Rum. 8:14; 3 Ne. 9:17; M&M 11:30). Sasa tu wana wa Mungu, 1 Yoh. 3:1–2. Mtaitwa watoto wa Kristo, wana na mabinti zake, Mos. 5:7. Watu wote ni lazima wazaliwe tena, ili kuwa wana na mabinti zake, Mos. 27:25. Watakuwa wana wangu na mabinti zangu, Eth. 3:14. Wewe hakika utafanyika mtoto wa Kristo, Moro. 7:19. Wale wote wenye kuipokea injili yangu ni wana na mabinti, M&M 25:1. Wao ni miungu, hata wana wa Mungu, M&M 76:58. Hivyo wote wapate kufanyika wana wangu, Musa 6:68. Wengi wameamini na wamekuwa wana wa Mungu, Musa 7:1.