Paka mafuta
Katika nyakati za kale, ni manabii wa Bwana waliwapaka kwa mafuta wale ambao wangetenda kazi maalumu, kama vile Haruni au makuhani au wafalme ambao wangeitawala Israeli. Katika Kanisa leo, kupaka ni kuweka kiasi kidogo cha mafuta yaliyotakaswa juu ya kichwa cha mtu kama sehemu ya baraka maalumu. Hii inaweza tu kufanywa chini ya mamlaka na nguvu za Ukuhani wa Melkizedeki. Baada ya mpako, mtu anayefanya chini ya mamlaka ya ukuhani huo huo anaweza kufunga mpako huo na kutoa baraka maalumu kwa yule aliyepakwa.