Adhabu Kuu Ona pia Mauaji Adhabu ya kifo kwa kosa la jinai lililotendeka, hususani linahusiana na adhabu ya kuua. Atakaye mwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, Mwa. 9:6 (TJS, Mwa. 9:12–13). Mwuaji hakika atauawa, Hes. 35:16. Wauaji wanaouwa kwa makusudi watakufa, 2 Ne. 9:35. Wewe umehukumiwa kufa kulingana na sheria, Alma 1:13–14. Yule aliyeua aliadhibiwa kwa kifo, Alma 1:18. Sheria inahitaji uhai wa yule aliyeua, Alma 34:12. Yule anayeua atakufa, M&M 42:19.