Haki ya uamuzi Ona pia Huru, Uhuru; Kuwajibika, Uwajibikaji, Wajibika Uwezo na nafasi Mungu awapayo watu ili kujichagulia na kutenda wao wenyewe. Mna uhuru wa kula kila mti, Mwa. 2:16. Chagueni hivi leo mtakayemtumikia, Yos. 24:15 (Alma 30:8; Musa 6:33). Mwanadamu asingeweza kujiamulia mwenyewe bila kuvutiwa, 2 Ne. 2:15–16. Wanadamu wako huru kuchagua uhuru na uzima wa milele, au utumwa na mauti, 2 Ne. 2:27. Ninyi mko huru; mmeruhusiwa kujichagulia wenyewe, Hel. 14:30. Theluthi moja ya majeshi ya mbinguni aliyageuza kwa sababu ya haki yao ya kujiamulia, M&M 29:36. Ilikuwa ni muhimu kwamba ibilisi awajaribu wanadamu, au la sivyo wasingeliweza kujiamulia wenyewe, M&M 29:39. Kila mtu na ajiamulie mwenyewe, M&M 37:4. Kila mtu aweza kutenda kulingana na haki ya kujiamulia niliyompatia, M&M 101:78. Shetani alitafuta kuiangamiza haki ya mwanadamu ya kujiamulia, Musa 4:3. Bwana akampatia mwanadamu haki yake ya uamuzi, Musa 7:32.