Katika Agano Jipya, ni bikira aliyechaguliwa na Mungu Baba kuwa mama wa Mwanawe katika mwili. Baada ya kuzaliwa kwa Yesu, Maria alipata watoto wengine (Mk. 6:3 ).
Aliposwa na Yusufu, Mt. 1:18 (Lk. 1:27 ).
Yusufu aliambiwa asimpe talaka Maria au asimfungue posa ile, Mt. 1:18–25 .
Mamajusi walimtembelea Maria, Mt. 2:11 .
Maria na Yusufu walikimbia pamoja na mtoto Yesu hadi Misri, Mt. 2:13–14 .
Baada ya kifo cha Herode, familia ilirejea Nazarethi, Mt. 2:19–23 .
Malaika Gabrieli alimtembelea, Lk. 1:26–38 .
Alimtembelea Elizabethi, binamu yake, Lk. 1:36, 40–45 .
Maria alitoa zaburi ya sifa kwa Bwana, Lk. 1:46–55 .
Maria alikwenda Bethlehemu pamoja na Yusufu, Lk. 2:4–5 .
Maria akamzaa Yesu na akamlaza horini, Lk. 2:7 .
Wachunga kondoo wakaenda Bethlehemu kumwona mtoto Yesu, Lk. 2:16–20 .
Maria na Yusufu walimpeleka Yesu hekaluni huko Yerusalemu, Lk. 2:21–38 .
Maria na Yusufu walimpeleka Yesu katika Pasaka, Lk. 2:41–52 .
Maria alikuwepo katika harusi huko Kana, Yn. 2:2–5 .
Mwokozi, alipokuwa juu ya msalaba, alimwomba Yohana amtunze mama yake, Yn. 19:25–27 .
Maria alikuwa pamoja na Mitume baada ya Yesu kutwaliwa mbinguni, Mdo. 1:14 .
Maria alikuwa bikira, mrembo sana na mwenye haki zaidi ya mabikira wengine wote, 1 Ne. 11:13–20 .
Mama wa Kristo angeitwa Maria, Mos. 3:8 .
Maria angekuwa bikira, mzuri na chombo kiteule, Alma 7:10 .