Ponya, Uponyaji Ona pia Huduma kwa Wagonjwa; Paka mafuta Kufanya mtu ajisikie vyema au kupata afya tena, kimwili na kiroho. Maandiko yana mifano mingi ya uponyaji wa kimiujiza wa Bwana na watumishi Wake. Mimi ni Bwana ambaye nimekuponya, Ku. 15:26. Naamani alijichovya yeye mwenyewe ndani ya Mto Yordani mara saba na akaponywa, 2 Fal. 5:1–14. Kwa fimbo zake tumeponywa, Isa. 53:5 (Mos. 14:5). Jua la walio na haki litachomoza na uponyaji katika mbawa zake, Mal. 4:2. Yesu aliponya aina zote za magonjwa, Mt. 4:23 (Mt. 9:35). Aliwapa uwezo wa kuponya aina zote za magonjwa, Mt. 10:1. Amenituma mimi kuwaponya waliovunjika moyo, Lk. 4:18. Waliponywa kwa uwezo wa Mwanakondoo wa Mungu, 1 Ne. 11:31. Kama unaamini katika ukombozi wa Kristo, unaweza ukaponywa, Alma 15:8. Aliwaponya kila mmoja, 3 Ne. 17:9. Yule aliye na imani nami ya kuponywa ataponywa, M&M 42:48. Katika jina langu watawaponya wagonjwa, M&M 84:68. Tunaamini katika karama ya uponyaji, M ya I 1:7.