Sauti Ona pia Ufunuo Kama inavyotumika katika maandiko, wakati mwingine ujumbe unaosikika ukisemwa na Bwana au wajumbe Wake. Sauti ya Roho yaweza pia kuwa isiyosikika na ikaelekezwa moyoni au akilini. Adamu na Hawa walisikia sauti ya Bwana Mungu, Mwa. 3:8 (Musa 4:14). Bwana alinena na Eliya katika sauti ndogo ya utulivu, 1 Fal. 19:11–13. Walio waadilifu huisikia sauti ya Mchungaji Mwema, Yn. 10:1–16. Kila mmoja aliye wa kweli huisikia sauti yangu, Yn. 18:37. Niliitii sauti ya Roho, 1 Ne. 4:6–18. Ikaja sauti kwangu, ikisema: Enoshi, dhambi zako zimesamehewa, Eno. 1:5. Ilikuwa sauti tulivu ya ulaini mkamilifu na ilipenya hata kwenye roho, Hel. 5:29–33 (3 Ne. 11:3–7). Iwe kwa sauti yangu mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, ni sawa, M&M 1:38. Lolote watakalosema wakati wanaongozwa na Roho Mtakatifu litakuwa sauti ya Bwana, M&M 68:2–4. Kila mtu ambaye hutii sauti yangu atauona uso wangu na kujua kuwa Mimi ndimi, M&M 93:1.