Husuda Ona pia Tamani; Wivu, enye Wivu Kulingana na maandiko, kutamani kitu fulani ambacho ni cha mtu mwingine ni kosa. Mapatriaki, walisukumwa na husuda, wakamwuza Yusufu katika Misri, Mdo. 7:9. Hisani haihusudu, 1 Kor. 13:4 (Moro. 7:45). Husuda hutokana na majivuno, 1 Tim. 6:4. Palipo na husuda ndipo palipo na machafuko na kila tendo ovu, Yak. (Bib.) 3:16. Bwana aliwaamuru wanadamu kwamba wasiwe na husuda, 2 Ne. 26:32. Hapakuwa na husuda miongoni mwa watu wa Nefi, 4 Ne. 1:15–18. Husuda na ghadhabu za wanadamu zimekuwa ni jambo la kawaida siku zote za maisha yangu, M&M 127:2.