Madhabahu Ona pia Dhabihu Kitu mfano wa meza kilichotumiwa kwa ajili ya kutolea dhabihu, matoleo, na kuabudu. Nuhu akamjengea Bwana madhabahu na akamtolea sadaka za kuteketezwa, Mwa. 8:20. Abramu akamjengea Bwana madhabahu, Mwa. 12:7–8. Ibrahimu akamfunga mwanawe Isaka juu ya madhabahu, Mwa. 22:9 (Mwa. 22:1–13). Yakobo akajenga hapo madhabahu na akapaita mahali pale Eli-Betheli, Mwa. 35:6–7. Eliya akajenga madhabahu na akawataka makuhani wa Baali kufanya vivyo hivyo, 1 Fal. 18:17–40. Ukileta sadaka yako madhabahuni, kwanza patana na ndugu yako, Mt. 5:23–24. Niliona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, Ufu. 6:9 (M&M 135:7). Lehi akajenga madhabahu ya mawe na akamtolea Mungu shukrani, 1 Ne. 2:7. Ibrahimu aliokolewa kutoka katika na mauti juu ya madhabahu ya Elkana, Ibr. 1:8–20.