Matendo Matendo ya mtu, yawe mabaya au mema. Kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake mwenyewe. Bwana atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake, Mit. 24:12. Nuru yenu na iangaze mbele za watu, ili wapate kuyaona matendo ya Mungu wenu, Mt. 5:16 (3 Ne. 12:16). Mtu yule atendaye mapenzi ya Baba ataingia katika ufalme wa mbinguni, Mt. 7:21. Imani pasipo matendo imekufa, Yak. (Bib.) 2:14–26. Lazima wahukumiwe juu ya matendo yao, 1 Ne. 15:32 (Mos. 3:24). Tunajua ya kuwa kwa neema tunaokolewa, baada ya kufanya yote tuwezayo kufanya, 2 Ne. 25:23. Wafundisheni kuwa kamwe wasichoke kufanya matendo mema, Alma 37:34. Ni lazima kwamba wanadamu wahukumiwe kulingana na matendo yao, Alma 41:3. Kwa matendo yao mtawajua, Moro. 7:5 (M&M 18:38). Mimi, Bwana, nitawahukumu watu wote kulingana na matendo yao, M&M 137:9.