Misaada ya Kujifunza
Moroni, Mwana wa Mormoni


Moroni, Mwana wa Mormoni

Nabii wa mwisho Mnefi katika Kitabu cha Mormoni (mnamo mwaka 421 B.K.). Muda mfupi kabla ya kifo cha Mormoni, yeye alikabidhi maandishi ya kihistoria yaliyoitwa mabamba ya Mormoni kwa mwanawe Moroni (M. ya Morm. 1:1). Moroni alimalizia kukusanya mabamba ya Mormoni. Aliongezea mlango wa 8 na wa 9 katika Kitabu cha Mormoni (Morm. 8:1). Aliandika kwa ufupi na kukiongeza Kitabu cha Etheri (Eth. 1:1–2) na akaongeza kitabu chake yeye mwenyewe kinachoitwa Kitabu cha Moroni (Moro. 1). Moroni aliyafunga mabamba hayo na akayaficha katika kilima Kumora (Morm. 8:14; Moro. 10:2). Katika mwaka 1823 Moroni alitumwa kama kiumbe mfufuka ili kukifunua Kitabu cha Mormoni kwa Joseph Smith (M&M 27:5; JS—H 1:30–42, 45). Alimfundisha nabii huyu kijana kila mwaka tangu mwaka 1823 hadi 1827 (JS—H 1:54) na mwishowe akayakabidhi mabamba kwake katika mwaka wa 1827 (JS—H 1:59). Baada ya kumaliza kutafsiri Joseph Smith aliyarudisha mabamba yale kwa Moroni.

Kitabu cha Moroni

Kitabu cha mwisho ndani ya Kitabu cha Mormoni. Kiliandikwa na nabii huyu wa mwisho Mnefi, Moroni. Mlango 1–3 husimulia juu ya angamizo la mwisho la Wanefi, kutoa maelekezo juu ya kutunukiwa kwa Roho Mtakatifu na ukuhani. Mlango wa 4–5 inaeleza kwa mapana namna sahihi ya kuhudumia sakramenti. Mlango wa 6 anafanya muhtasari wa kazi ya Kanisa. Mlango 7–8 ni mafundisho juu ya kanuni za kwanza za injili, pamoja na mafundisho ya Mormoni juu ya imani, tumaini, na hisani na jinsi ya kuhukumu mema na maovu (Moro. 7), na maelezo ya Mormoni kwamba watoto wadogo wako hai katika Kristo na hawahitaji ubatizo (Moro. 8). Mlango wa 9 huelezea kutemwa kwa taifa la Wanefi. Mlango wa 10 ni ujumbe wa mwisho wa Moroni na unajumuisha njia ya kujua ukweli wa Kitabu cha Mormoni (Moro. 10:3–5).