Kuwa mwenye haki, mtakatifu, wema, wima, unyofu, uaminifu; kutenda katika utii kwa amri za Mungu; kuepuka dhambi.
Matokeo yasiyotindika ya baraka kwa ajili ya mawazo na matendo ya uadilifu, na adhabu kwa dhambi zisizofanyiwa toba. Haki ni sheria ya milele ambayo huhitaji adhabu kila mara sheria ya Mungu inapovunjwa (Alma 42:13–24 ). Mtenda dhambi ni lazima alipe adhabu kama hatubu (Mos. 2:38–39 ; M&M 19:17 ). Kama anatubu, Mwokozi humlipia ile adhabu kupitia upatanisho kwa kuomba rehema (Alma 34:16 ).
Hadi nitakapokufa, sitajiondelea uadilifu wangu, Ayu. 27:5 .
Bwana atawabariki wenye haki, Zab. 5:12 .
Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Zab. 34:15, 17 (1Â Pet. 3:12 ).
Mwenye haki huenda katika uadilifu wake, Mit. 20:7 .
Wakati wenye haki wawapo katika mamlaka, watu hufurahi, Mit. 29:2 (M&M 98:9–10 ).
Roho ile itendayo dhambi itakufa, Eze. 18:4 .
Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, Mika 6:8 .
Haki ya Mungu iliwatenga waovu na wenye haki, 1Â Ne. 15:30 .
Aliye na haki hupendelewa na Mungu, 1Â Ne. 17:35 .
Atawalinda wenye haki; hawahitaji kuogopa, 1Â Ne. 22:17, 22 .
Shetani hatakuwa na nguvu kwa sababu ya uadilifu wa watu wa Bwana, 1Â Ne. 22:26 .
Kama hakutakuwa na uadilifu hapatakuwepo na furaha, 2Â Ne. 2:13 .
Wenye haki wataurithi ufalme wa Mungu, 2Â Ne. 9:18 .
Upatanisho hutosheleza mahitaji ya haki yake, 2Â Ne. 9:26 .
Wenye haki hawaogopi maneno ya kweli, 2Â Ne. 9:40 .
Watu wote lazima wabadilike na kuwa katika hali ya uadilifu, Mos. 27:25–26 .
Majina ya wenye haki yataandikwa katika kitabu cha uzima, Alma 5:58 .
Wanadamu wote wameanguka na wameshikwa na haki, Alma 42:14 .
Upatanisho huridhisha mahitaji ya haki, Alma 42:15 .
Ninyi mwadhani rehema yaweza kuiibia haki, Alma 42:25 .
Walikuwa watu waliokuwa wakweli katika nyakati zote na katika mambo yote waliyoaminiwa, Alma 53:20 .
Haki ya Mungu huningʼinia juu yako isipokuwa utubu, Alma 54:6 .
Mmetafuta furaha kwa kufanya uovu, kitu ambacho ni kinyume cha asili ya uadilifu, Hel. 13:38 .
Wimbo wa mwenye haki ni sala kwangu, M&M 25:12 .
Simama ukiwa umevaa dirii ya uadilifu, M&M 27:16 (Efe. 6:14 ).
Mauti ya wenye haki ni matamu kwao, M&M 42:46 .
Wenye haki watakusanywa kutoka miongoni mwa mataifa yote, M&M 45:71 .
Wanadamu wanapaswa kutenda mengi ya uadilifu kwa mapenzi yao wenyewe, M&M 58:27 .
Yule afanyaye matendo ya uadilifu atapokea amani katika ulimwengu huu na uzima wa milele katika ulimwengu ujao, M&M 59:23 .
Katika Ujio wa Pili, kutakuwako utengano mkamilifu wa wenye haki na wale waovu, M&M 63:54 .
Haki na hukumu ni adhabu zilizowekwa kwa sheria yangu, M&M 82:4 .
Haki huchukua mkondo wake na kudai chake, M&M 88:40 .
Hakuna atakayesamehewa kutokana na haki na sheria za Mungu, M&M 107:84 .
Nguvu za mbinguni zaweza kudhibitiwa tu juu ya kanuni za uadilifu, M&M 121:36 .
Bwana alimpenda Hyrum Smith kwa sababu ya uadilifu wa moyo wake, M&M 124:15 .
Miongoni mwa wenye haki palikuwepo na amani, M&M 138:22 .
Watu wa Sayuni waliishi katika uadilifu, Musa 7:18 .
Ibrahimu alikuwa mfuasi wa uadilifu, Ibr. 1:2 .