Misaada ya Kujifunza
Sala


Sala

Mawasiliano ya unyenyekevu kati ya mtu na Mungu wakati ambapo mtu hutoa shukrani na kuomba baraka. Sala hutolewa kwa Baba wa Mbinguni katika jina la Yesu Kristo. Sala zaweza kusemwa kwa sauti au kimya kimya. Mawazo ya mtu yaweza pia kuwa sala kama yanaelekezwa kwa Mungu. Wimbo wa mwenye haki waweza kuwa sala kwa Mungu (M&M 25:12).

Madhumuni ya sala siyo kubadilisha mapenzi ya Mungu, bali kujipatia kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajili ya wengine baraka ambazo Mungu tayari anataka kutupa, lakini tunalazimika kuomba ili tuweze kuzipata.

Tunasali kwa Baba katika jina la Kristo (Yn. 14:13–14; 16:23–24). Hakika tunaweza kusali katika jina la Yesu wakati matakwa yetu yanapokuwa matakwa ya Kristo (Yn. 15:7; M&M 46:30). Kisha tunaomba mambo yale yaliyo sahihi na hivyo Mungu huwa radhi kutupatia (3 Ne. 18:20). Sala zingine hubaki pasipo kujibiwa kwa sababu kwa njia yoyote ile hayawakilishi matakwa ya Kristo bali badala yake hutokana na ubinafsi wa mtu huyo (Yak. [Bib.] 4:3; M&M 46:9). Kweli, kama tutamwomba Mungu mambo yasiyo ya haki, yatageuka kuwa lana kwetu (M&M 88:65).