Upenzi na urafiki wa kina. Upendo kwa Mungu ni pamoja na kupenda kwa moyo, kuabudu, heshima kuu, upole, rehema, msamaha, huruma, neema, huduma, shukrani, wema. Mfano mkuu wa upendo wa Mungu kwa watoto wake unaonekana katika Upatanisho usio na mwisho wa Yesu Kristo.
Jinsi gani Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa Pekee, Yn. 3:16 (M&M 138:3 ).
Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi, Yn. 13:34 (Yn. 15:12, 17 ; Musa 7:33 ).
Kama mnanipenda, zishikeni amri zangu, Yn. 14:15 (M&M 42:29 ).
Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kana huu, kwamba ananatoa maisha yake kwa marafiki zake, Yn. 15:13 .
Petro, wanipenda kuliko hawa? Lisha kondoo wangu, Yn. 21:15–17 .
Hakuna kitu kitakachotutenga sisi na upendo wa Mungu ulio katika Kristo, Rum. 8:35–39 .
Jicho halijaona mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao, 1Â Kor. 2:9 .
Tumikianeni kwa upendo, Gal. 5:13 .
Waume, wapendeni wake zenu, Efe. 5:25 (Kol. 3:19 ).
Msiipende dunia, 1Â Yoh. 2:15 .
Mungu ni upendo, 1Â Yoh. 4:8 .
Sisi twampenda, kwa sababu yeye alitupenda sisi kwanza, 1Â Yoh. 4:19 .
Kristo huteseka kwa sababu ya wema wa upendo wake kwa wanadamu, 1Â Ne. 19:9 .
Songeni mbele kwa upendo wa Mungu na wa wanadamu wote, 2Â Ne. 31:20 .
Mtawafundisha watoto wenu kupendana na kutumikiana, Mos. 4:15 .
Kama mmejisikia kuimba wimbo wa upendo wa ukombozi, mwaweza kujisikia hivyo hivi sasa, Alma 5:26 .
Mkaongozwe na Roho Mtakatifu, katika kuwa wenye subira, waliojawa na upendo, Alma 13:28 .
Zuia tamaa zako zote, ili upate kujawa na upendo, Alma 38:12 .
Hapakuwa na ubishi kwa sababu ya upendo wa Mungu uliokaa katika mioyo ya watu, 4Â Ne. 1:15 .
Kila kitu kikaribishacho kumpenda Mungu kimeongozwa na Mungu, Moro. 7:13–16 .
Hisani ni upendo safi wa Kristo, Moro. 7:47 .
Pendo kamili huitupa nje hofu, Moro. 8:16 (1Â Yoh. 4:18 ).
Upendo huwapasisha wanadamu katika kazi ya Mungu, M&M 4:5 (M&M 12:8 ).
Utakaso huja kwa wale wote wenye kumpenda na kumtumikia Mungu, M&M 20:31 .
Kama wanipenda, utanitumikia na kushika amri zangu, M&M 42:29 (Yn. 14:15 ).
Onyesha ongezeko la upendo kwa wale unaowasahihisha au kuwakemea, M&M 121:43 .