Pumzika Ona pia Amani; Siku ya Sabato Kufurahia amani na uhuru kwa kuondokana na usumbufu na ghasia. Bwana ameahidi hivyo kwa wafuasi wake walio waaminifu katika maisha haya. Pia ameandaa mahali pa pumziko kwa ajili yao katika maisha yajayo. Uwepo wangu utakwenda pamoja nanyi, nami nitawapa pumziko, Ku. 33:14. Njooni kwangu, ninyi nyote wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha, Mt. 11:28–29. Tulifanya kazi kwa bidii ili wapate kuingia katika pumziko lake, Yak. (KM) 1:7 (Ebr. 4:1–11). Yeyote atakayetubu ataingia katika pumziko langu, Alma 12:34. Kulikuwa na wengi kupita kiasi, waliotakaswa, na wakaingia katika pumziko la Bwana, Alma 13:12–16. Peponi ni hali ya pumziko, Alma 40:12 (Alma 60:13). Hakuna kiingiacho katika pumziko lake isipokuwa wale walioosha mavazi yao katika damu yangu, 3 Ne. 27:19. Tangaza toba kwa watu hawa, ili upate kupumzika pamoja nao katika ufalme wa Baba yangu, M&M 15:6 (M&M 16:6). Wale wanaokufa watapumzika baada ya kazi zao zote, M&M 59:2 (Ufu. 14:13). Pumziko la Bwana ni utimilifu wa utukufu wake, M&M 84:24.