Hekima Ona pia Maarifa; Ufahamu; Ukweli Uwezo au kipawa kutoka kwa Mungu cha kuhukumu kwa usahihi. Mtu hupata hekima kwa njia ya uzoefu na kujifunza na kwa kufuata ushauri wa Mungu. Pasipo msaada wa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa na hekima ya kweli (2 Ne. 9:28; 27:26). Mungu alimpa Sulemani hekima, 1 Fal. 4:29–30. Hekima ndicho kitu muhimu; kwa hiyo jipatie hekima, Mit. 4:7. Apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, Mit. 19:8. Yesu aliongezeka hekima, Lk. 2:40, 52. Kama mtu yeyote kati yenu akipungukiwa na hekima, na aombe kwa Mungu, Yak. (Bib.) 1:5 (M&M 42:68; JS—H 1:11). Ninawaambia mambo haya ili mpate kujifunza kuwa na hekima, Mos. 2:17. Jifunze hekima katika ujana wako, Alma 37:35. Watakatifu watapata hekima na hazina kuu ya maarifa, M&M 89:19. Acheni yule ambaye yu mjinga ajifunze hekima kwa kujinyenyekeza mwenyewe na kumlingana Bwana, M&M 136:32.