Askofu Kiongozi Kiongozi Mkuu katika Kanisa. Anao wajibu mkuu juu ya mambo ya ustawi wa Kanisa (M&M 107:68). Askofu Kiongozi na washauri wake, ambao pia ni Viongozi Wakuu, huongoza juu ya Ukuhani wa Haruni wa Kanisa (M&M 68:16–17; 107:76, 87–88). Edward Partridge atawazwa kuwa askofu, M&M 41:9. Maaskofu wataitwa na kutegwa rasmi na Urais wa Kwanza, M&M 68:14–15. Wazawa halisi wa Haruni, walio wazaliwa wa kwanza, wanayo haki ya kuongoza kama wataitwa, kutengwa rasmi, na kutawazwa na Urais wa Kwanza, M&M 68:16, 18–20. Aweza kushtakiwa tu mbele ya Urais wa Kwanza, M&M 68:22–24 (M&M 107:82).