Danganya, Kudanganya, Udanganyifu Ona pia Hila; Kusema uongo Katika maandiko, kudanganya ni kusababisha mtu aamini kitu ambacho si cha kweli. Yule asiyeapa kwa hila atapanda katika mlima wa Bwana, Zab. 24:3–4. Uniokoe na mtu wa hila, Zab. 43:1. Ole wao waitao uovu ni wema, na wema ni uovu, Isa. 5:20 (2 Ne. 15:20). Na mtu asijidanganye mwenyewe, 1 Kor. 3:18. Na mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana, Efe. 5:6. Watu waovu watadanganya na watadanganyika, 2 Tim. 3:13. Shetani, ambaye aliudanganya ulimwengu wote, alitupwa nje, Ufu. 12:9. Shetani alifungwa ili asipate kuwadanganya tena mataifa, Ufu. 20:1–3. Bwana hawezi kudanganywa, 2 Ne. 9:41. Kama mtamfuata Mwana, pasipo kutenda udanganyifu mbele za Mungu, mtampokea Roho Mtakatifu, 2 Ne. 31:13. Sheremu alikiri kwamba alidanganywa kwa nguvu za ibilisi, Yak. (KM) 7:18. Watu wa Mfalme Nuhu walidanganywa kwa maneno ya ulaghai, Mos. 11:7. Wenye hekima wamemchukua Roho Mtakatifu kuwa kiongozi wao, nao hawajadanganyika, M&M 45:57. Ole wao wale walio wadanganyifu, M&M 50:6. Akawa Shetani, baba wa uongo wote, kudanganya na kuwapofusha wanadamu, Musa 4:4.