Mafundisho ya Kristo Ona pia Injili; Mpango wa Ukombozi Kanuni na mafundisho ya injili ya Yesu Kristo. Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Kum. 32:2. Hao wanungʼunikao watajifunza elimu, Isa. 29:24. Watu walishangaa mno kwa mafundisho yake, Mt. 7:28. Mafundisho yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenituma, Yn. 7:16. Kila andiko lafaa kwa mafundisho, 2 Tim. 3:16. Hili ndilo fundisho la Kristo, na ndilo fundisho pekee na la kweli la Baba, 2 Ne. 31:21 (2 Ne. 32:6). Hapatakuwa na ugomvi miongoni mwenu kuhusu mambo ya mafundisho yangu, 3 Ne. 11:28, 32, 35, 39–40. Shetani huichochea mioyo ya watu ili wabishe kuhusu mambo ya mafundisho yangu, M&M 10:62–63, 67. Wafundisheni watoto mafundisho ya toba, imani katika Kristo, ubatizo, na kipawa cha Roho Mtakatifu, M&M 68:25. Fundishaneni mafundisho ya ufalme, M&M 88:77–78. Mafundisho ya ukuhani yatatonatona juu ya roho yako, M&M 121:45.