Tegemea Ona pia Amini, Imani; Matumaini Kutegemea au kuweka matumaini yako katika mtu fulani au jambo fulani. Katika mambo ya kiroho, kutegemea kunajumuisha kumtegemea Mungu na Roho Wake. Japo kuwa ataniua, bado nitamtumaini yeye, Ayu. 13:15. Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Mit. 3:5. Bwana aliwaokoa watumishi wake ambao walimtumaini yeye, Dan. 3:19–28. Nitakutumaini wewe milele, 2 Ne. 4:34. Furahini na kuweka matumaini yenu katika Mungu, Mos. 7:19. Mtu yeyote awekaye tumaini lake katika Mungu atainuliwa katika ile siku ya mwisho, Mos. 23:22. Watu wowote watakao mwamini Mungu watasaidiwa katika majaribu yao, Alma 36:3, 27. Usiuegemee mkono wa mwanadamu, M&M 1:19. Weka imani yako katika ile Roho ambayo hutuongoza kufanya yaliyo mema, M&M 11:12. Mwache anitumaini mimi, naye hatashindwa, M&M 84:116.