Kamilifu Kamili, nzima, na iliyo komaa; adilifu kabisa. Kamilifu inaweza pia kumaanisha pasipo dhambi au uovu. Ni Kristo pekee ndiye aliyekuwa mkamilifu kabisa. Wafuasi wa kweli wa Kristo wanaweza kuwa wakamilifu kwa njia ya neema na Upatanisho Wake. Mioyo yenu na iwe kamili kwa Bwana, 1 Fal. 8:61. Basi ninyi mtakuwa wakamilifu hata kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu, Mt. 5:48 (3 Ne. 12:48). Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, Yak. (Bib.) 3:2. Imani sio kuwa na ufahamu mkamilifu juu ya mambo, Alma 32:21, 26. Upatanisho ulifanyika ili Mungu apate kuwa Mungu mkamilifu, Alma 42:15. Moroni alikuwa mtu mwenye ufahamu mkamilifu, Alma 48:11–13, 17–18. Roho ya Kristo imetolewa kwa kila mtu ili apate kuhukumu na kujua kwa ufahamu kamili ikiwa kitu fulani ni cha Mungu au cha ibilisi, Moro. 7:15–17. Njooni kwa Kristo, na mkakamilike ndani yake, Moro. 10:32. Endeleeni katika subira hadi mtakapokuwa mmekamilika, M&M 67:13. Hawa ndiyo wale watu wenye haki waliokamilishwa kwa njia ya Yesu, M&M 76:69. Ofisi zilizoko katika Kanisa ni kwa ajili ya kuwakamilisha Watakatifu, M&M 124:143 (Efe. 4:11–13). Walio hai hawakamiliki pasipo wafu wao, M&M 128:15, 18. Nuhu alikuwa mtu mwenye haki, na mkamilifu katika kizazi chake, Musa 8:27.