Tamani Ona pia Husuda Kama lilivyotumika katika maandiko, kutamani ni kumwonea wivu mtu fulani au kuwa na tamaa kupita kiasi kwa ajili ya kitu fulani. Usitamani, Ku. 20:17 (Kum. 5:21; Mos. 13:24; M&M 19:25). Yule achukiaye kutamani ataongeza siku zake, Mit. 28:16. Hutamani mashamba na kuyashika, Mik. 2:2. Jilindeni na choyo, Lk. 12:15. Torati ilisema, Usitamani, Rum. 7:7. Katika siku za mwisho, wanadamu watakuwa wenye tamaa, 2 Tim. 3:1–2. Labani alipoiona mali yetu, aliitamani, 1 Ne. 3:25. Usitamani mali yako wewe mwenyewe, M&M 19:26. Acheni kuwa na tamaa, M&M 88:123. Usitamani kile kilicho cha ndugu yako, M&M 136:20.