Misaada ya Kujifunza
Safi na Isiyo safi


Safi na Isiyo safi

Katika Agano la Kale, Bwana alimfunulia Musa na Waisraeli wa kale kwamba ni baadhi ya vyakula fulani tu vilionekana kuwa safi, au kwa maneno mengine, kufaa kuliwa. Tofauti ambayo Waisraeli waliifanya kati ya vyakula safi na visivyo safi ilikuwa na athari kubwa juu ya maisha yao ya kidini na kijamii. Baadhi ya wanyama, ndege na samaki walionekana kama ni safi na walikubalika kuliwa wakati wengine walikuwa siyo safi na walikatazwa (Law. 11; Kum. 14:3–20). Baadhi ya watu waliokuwa na ugonjwa fulani pia walifikiriwa kuwa siyo watu safi.

Katika mtazamo wa kiroho, kuwa safi ni kuwa bila dhambi na tamaa za kidhambi. Katika mtazamo huu neno hili linatumika kumwelezea mtu ambaye ni mwema na mwenye moyo mweupe (Zab. 24:4). Watu wa Mungu walio wa agano daima wamekuwa na mafundisho maalumu ili kuwa safi (3 Ne. 20:41; M&M 38:42; 133:5). Mtu aliyetenda dhambi anaweza kuwa safi kupitia imani katika Yesu Kristo, toba, na kupokea ibada za injili.