Isiyo kufa, Maisha ya kutokufa Ona pia Hali ya Kufa, enye Kufa; Lipia dhambi, Upatanisho; Ufufuko; Wokovu; Yesu Kristo Hali ya kuishi milele katika hali ya aliyefufuka, kutokuwa tena chini ya kifo cha kimwili. Amefufuka, Mk. 16:6. Kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa, 1 Kor. 15:22. Mauti humezwa wakati huu wa kufa utakapovaa kutokufa, 1 Kor. 15:53–54. Kristo ameishinda mauti na kuleta hali ya kutokufa, 2 Tim. 1:10. Hali ya kutokufa ni kurejeshwa kwa roho katika mwili, 2 Ne. 9:13. Roho zikiunganika pamoja na miili yao huwa na hali ya kutokufa, kamwe haifi tena, Alma 11:45. Watu walio waaminifu watavikwa taji la hali ya kutokufa na uzima wa milele, M&M 75:5. Dunia itatakaswa na kuwa isiyo kufa, M&M 77:1 (M&M 130:9). Kazi na utukufu wa Mungu ni kuleta hali ya kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu, Musa 1:39.