Mwamba Ona pia Injili; Ufunuo; Yesu Kristo Kitaswira, Yesu Kristo na injili Yake, ambao ndiyo msingi na msaada imara (M&M 11:24; 33:12–13). Mwamba pia waweza kumaanisha ufunuo, ambao kwa huo Mungu hufanya injili Yake ijulikane kwa wanadamu (Mt. 16:15–18). Yeye ni mwamba, kazi yake ni kamilifu, Kum. 32:4. Bwana ni mwamba wangu; nitamwamini yeye, 2 Sam. 22:2–3. Jiwe likachongwa pasipo mikono, Dan. 2:34–35. Msingi wake ulijengwa juu ya mwamba, Mt. 7:25 (3 Ne. 14:25). Yesu Kristo ndiye jiwe lile ambalo lilidharauliwa, Mdo. 4:10–11. Mwamba ule ulikuwa Kristo, 1 Kor. 10:1–4 (Ku. 17:6). Yule aliyejengwa juu ya mwamba huupokea ukweli, 2 Ne. 28:28. Wayahudi watalikataa lile jiwe [Kristo] ambalo juu yake wangelijenga, Yak. (KM) 4:15–17. Ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu kwamba ni lazima tujenge msingi wetu, Hel. 5:12. Yeyote ajengaye juu ya mafundisho ya Kristo hujenga juu ya mwamba wake naye hataanguka wakati mafuriko yatakapokuja, 3 Ne. 11:39–40 (Mt. 7:24–27; 3 Ne. 18:12–13). Mtu mwenye hekima alijenga nyumba yake juu ya mwamba, 3 Ne. 14:24. Kama mmejengwa juu ya mwamba wangu, dunia na jehanamu hazitawashinda, M&M 6:34. Yule ajengaye juu ya mwamba huu hataanguka kamwe, M&M 50:44. Mimi ndimi Masiya, Mfalme wa Sayuni, Mwamba wa Mbinguni, Musa 7:53.