Rehoboamu
Katika Agano la Kale, ni mwana wa Mfalme Suleimani. Alimrithi baba yake na alitawala kwa miaka kumi na saba katika Yerusalemu (1 Fal. 11:43; 14:21, 31). Wakati wa utawala wa Rehoboamu, ufalme uligawanyika katika ufalme wa Israeli ya kaskazini na ufalme wa Yuda kusini (1 Fal. 11:31–36; 12:19–20). Rehoboamu alitawala ufalme wa Yuda.