Wafilisti
Katika Agano la Kale, ni kabila ambalo kwa asili lilikuja kutoka Kaftari (Amo. 9:7) na wakakaa katika bonde tajiri juu ya pwani ya Mediterania kuanzia Yafa hadi jangwa la Misri kabla ya siku za Ibrahimu (Mwa. 21:32). Kwa miaka mingi palikuwepo vita vya kijeshi kati ya Wafilisti na Waisraeli. Hatimaye Palestina, jina la dola ya Wafilisti, limekuwa jina maarufu kwa Nchi yote Takatifu.