Ovu, Uovu Ona pia Chafu, Uchafu; Dhambi; Giza, Kiroho; Kutokuwa Adilifu, Siyo Adilifu; Sio mcha mungu Dhambi; kutokuwa mtiifu kwa amri za Mungu. Nawezaje basi kutenda uovu huu mkubwa, na kutenda dhambi kwa Mungu, Mwa. 39:7–9. Bwana yu mbali na wasio na haki: bali husikia sala ya wenye haki, Mit. 15:29. Mwovu anapotawala, watu huugua, Mit. 29:2 (M&M 98:9). Mwondoeni mtu mwovu miongoni mwenu, 1 Kor. 5:13. Tunashindana na uovu wa kiroho katika mahali pa juu, Efe. 6:12. Tokeni nje kutoka kwa waovu, na msiguse vitu vyao visivyo safi, Alma 5:56–57 (M&M 38:42). Hii ndiyo hali ya mwisho ya waovu, Alma 34:35 (Alma 40:13–14). Kamwe uovu haujapata kuwa furaha, Alma 41:10. Kwa njia ya waovu, waovu huadhibiwa, Morm. 4:5 (M&M 63:33). Katika saa hiyo waja utengano mkamilifu wa wenye haki na waovu, M&M 63:54. Hivyo waja mwisho wa waovu, JS—M 1:55.