Tohara
Ishara ya Agano la Ibrahimu kwa Waisraeli wanaume wakati wa kipindi cha Agano la Kale (Mwa. 17:10–11, 23–27; TJS, Mwa. 17:11 [Kiambatisho]). Tohara ilikuwa ikifanyika kwa kukata “ngozi ya mbeleni” ya mtoto mchanga wa kiume na pia mwanamume mtu mzima. Wale waliofanyiwa walifurahia heshima na kupokea kazi za agano. Tohara kama ishara ya agano ilifutwa kwa misheni ya Kristo (Moro. 8:8; M&M 74:3–7).