Haruni, Mwana wa Mosia Ona pia Mosia, Mwana wa Benjamini; Mosia, Wana wa Katika Kitabu cha Mormoni, ni mwana wa Mfalme Mosia. Haruni alitumika kama mmisionari ambaye jitihada zake zilisaidia kuziongoa roho za wengi kuja kwa Kristo. Alikuwa ni mtu asiyeamini aliyetafuta kuliangamiza Kanisa, Mos. 27:8–10, 34. Malaika aliwatokea yeye na wenzi wake, Mos. 27:11. Wakatubu na kuanza kulihubiri neno la Mungu, Mos. 27:32–28:8. Alikataa kuitwa mfalme na badala yake alikwenda katika nchi ya Walamani kuhubiri neno la Mungu, Alma 17:6–9. Akafunga na kusali ili kupata mwongozo, Alma 17:8–11. Alimfundisha baba wa Mfalme Lamoni, Alma 22:1–26. Alikwenda kuhubiri kwa Wazorami, Alma 31:6–7.