Mika
Nabii wa Agano la Kale. Alikuwa mwenyeji wa Moresheth-Ghathi, katika nchi tambarare ya Yuda, naye alitoa unabii wakati Hezekia alipokuwa mfalme (Mika 1:1–2).
Kitabu cha Mika
Mika ndicho kitabu pekee katika Agano la Kale kinachotaja Bethlehemu kama mahali ambapo Masiya angezaliwa (Mika 5:2). Katika kitabu hiki Bwana anasemezana na watu Wake na kukumbusha wema wake uliopita kwao; Yeye alihitaji haki, huruma, na unyenyekevu kutoka kwao (Mika 6:8).