Nia Welekevu wa akili; uwezo wa kufahamu fikira. Umtumikie kwa moyo mkamilifu na kwa nia ya kumkubali, 1Â Nya. 28:9. Mpende Bwana Mungu wako kwa akili zako zote, Mt. 22:37. Kufikiria kimwili ni kifo; kufikiria kiroho ni uzima wa milele, 2Â Ne. 9:39. Sauti ya Bwana ilinijia akilini mwangu, Eno. 1:10. Neno likawa matokeo na nguvu zaidi akilini mwa watu kuliko upanga, Alma 31:5. Nitakujulisha wewe akilini mwako, M&M 8:2. Lichunguze katika akili yako, M&M 9:8. Acha taadhima ya milele na iwe akilini mwenu, M&M 43:34. Akili zenu katika wakati uliopita zilitiwa giza, M&M 84:54. Laleni vitandani mwenu mapema, amkeni mapema ili miili yenu na akili zenu zipate kutiwa nguvu, M&M 88:124. Shetani hakujua mawazo ya Mungu, Musa 4:6. Bwana aliwaita watu wake Sayuni, kwa sababu walikuwa na moyo mmoja na nia moja, Musa 7:18.