Mwanzo, Kitabu cha Biblia
Kitabu cha Mwanzo ndiyo kitabu cha kwanza cha Agano la Kale na kiliandikwa na Nabii Musa. Kinatoa historia ya mianzo mingi ya mambo, kama vile uumbaji wa dunia, kuwekwa kwa wanyama na mwanadamu juu ya dunia, anguko la Adamu na Hawa, kufunuliwa kwa injili kwa Adamu, mwanzo wa makabila na jamii, asili ya lugha mbalimbali katika Babeli, na mwanzo wa familia ya Ibrahimu inayoongoza kuanzishwa kwa nyumba ya Israeli. Nafasi ya Yusufu kama mhifadhi wa Israeli inadhihirishwa katika Mwanzo.
Ufunuo wa siku za mwisho unathibitisha na kubainisha taarifa iliyoandikwa katika Mwanzo (1 Ne. 5; Eth. 1; Musa 1–8; Ibr. 1–5).
Katika Kitabu cha Mwanzo, mlango wa 1–4 inahusisha uumbaji wa ulimwengu na kukua kwa familia ya Adamu. Mlango wa 5–10 inaandika historia ya Nuhu. Mlango wa 11–20 inamtaja Ibrahimu na familia yake hadi wakati wa Isaka. Mlango wa 21–35 inafuatilia familia ya Isaka. Mlango wa 36 unasimulia juu ya Esau na familia yake. Mlango wa 37–50 inasimulia juu ya familia ya Yakobo na kutoa historia ya Yusufu kuuzwa Misri na nafasi yake katika kuiokoa nyumba ya Israeli.