Kiri, Kukiri
Maandiko hutumia neno kukiri katika njia zipatazo mbili. Katika maana moja, kukiri ni mtu kueleza imani yake katika kitu fulani, kama vile kukiri kwamba Yesu ndiye Kristo (Mt. 10:32; Rum. 10:9; 1 Yoh. 4:1–3; M&M 88:104).
Katika maana nyingine, kukiri ni mtu kukubali hatia, kama vile katika maungamo ya dhambi. Ni wajibu wa watu wote kuungama dhambi zao kwa Bwana na kupata msamaha Wake (M&M 58:42–43). Inapokuwa muhimu, dhambi yapaswa zikiriwa kwa mtu au watu uliowakosea. Dhambi kubwa yapaswa zikiriwe kwa viongozi wa Kanisa (hasa askofu).