Patriaki na nabii wa Agano la Kale; ni mdogo kati ya wana mapacha wa Isaka na Rebeka (Mwa. 25:19–26). Yakobo alipata haki ya uzaliwa wa kwanza dhidi ya kaka yake Esau. Hii ilikuwa kwa sababu ya ustahilivu wa Yakobo na kuoa katika agano, wakati Esau alikuwa akidharau haki yake ya uzaliwa wa kwanza na akaoa nje ya agano (Mwa. 25:30–34; 26:34–35; 27; 28:6–9; Ebr. 12:16).