Hali ya furaha kuu inayokuja kutokana na maisha ya uadilifu. Madhumuni ya maisha katika mwili wenye kufa ni kwa watu wote kuwa na shangwe (2 Ne. 2:22–25 ). shangwe kamilifu itakuja tu kupitia kwa Yesu Kristo (Yn. 15:11 ; M&M 93:33–34 ; 101:36 ).
Ninakuletea habari njema ya shangwe kuu, Lk. 2:10 .
shangwe yenu hakuna mtu awaondoleaye, Yn. 16:22 .
Tunda la Roho ni upendo, shangwe, amani, Gal. 5:22 .
Tunda lake lilijaza nafsi yangu kwa shangwe isiyo kifani, 1Â Ne. 8:12 .
Wanadamu wapo ili wapate kuwa na shangwe, 2Â Ne. 2:25 .
shangwe ya waadilifu itakuwa tele milele, 2Â Ne. 9:18 .
Wataweza kukaa na Mungu katika hali ya furaha isiyo na mwisho, Mos. 2:41 .
Nitaachia yote ninayo yamiliki ili nipate kupokea shangwe hii iliyo kuu, Alma 22:15 .
Huenda nikawa chombo mikononi mwa Mungu kuzileta baadhi ya nafsi kwenye toba, na hii ndiyo shangwe yangu, Alma 29:9 .
Ni shangwe gani, na nuru gani ya maajabu niliyoiona, Alma 36:20 .
Roho wangu ataijaza nafsi yako kwa shangwe, M&M 11:13 .
Shangwe itakuwa kubwa namna gani pamoja naye katika ufalme wa Baba yangu, M&M 18:15–16 .
Katika ulimwengu huu furaha yenu si kamilifu, bali ndani yangu shangwe yenu ni kamilifu, M&M 101:36 .