Pole, Upole Ona pia Mnyenyekevu, Unyenyekevu; Moyo Uliovunjika; Subira Mchamungu, mwadilifu, mnyenyekevu, mwenye kufundishika, na mvumilivu chini ya mateso. Watu wapole wako radhi kufuata mafundisho ya injili. Musa alikuwa mpole sana, Hes. 12:3. Wapole watairithi dunia, Zab. 37:11 (Mt. 5:5; 3 Ne. 12:5; M&M 88:17). Mtafuteni Bwana, enyi wote mlio wapole; itafuteni haki, tafuteni unyenyekevu, Sef. 2:3 (1 Tim. 6:11). Jifunzeni kwangu kwa kuwa Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, Mt. 11:29. Upole ni tunda la Roho, Gal. 5:22–23. Mtumishi wa Bwana lazima awe muungwana, awezaye kufundisha, mvumilivu, akiwaelekeza kwa upole wale wampingao, 2 Tim. 2:24–25. Roho ya upole na utulivu ni ya thamani kuu mbele za Mungu, 1 Pet. 3:4. Uvueni uanadamu wa asili na kuweni wanyenyekevu, Mos. 3:19 (Alma 13:27–28). Mungu alimwamuru Helamani kuwafundisha watu kuwa wapole, Alma 37:33. Neema ya Bwana yatosha kwa walio wanyenyekevu, Eth. 12:26. Mnayo imani katika Kristo kwa sababu ya unyenyekevu wenu, Moro. 7:39. Hakuna yeyote anayekubalika mbele za Mungu isipokuwa wapole na wanyenyekevu wa moyo, Moro. 7:44. Ondoleo la dhambi huleta unyenyekevu, na kwa sababu ya unyenyekevu huja kujiliwa na Roho Mtakatifu, Moro. 8:26. Enenda katika unyenyekevu wa Roho wangu, M&M 19:23. Tawala nyumba yako kwa unyenyekevu, M&M 31:9. Nguvu na uwezo wa Ukuhani vyaweza kudumishwa kwa upole na unyenyekevu, M&M 121:41.