Hamu Ona pia Nuhu, Patriaki wa Biblia Katika Agano la Kale, ni mwana wa tatu wa Nuhu (Mwa. 5:32; 6:10; Musa 8:12, 27). Nuhu, wanawe, na familia zao wakaingia katika safina, Mwa. 7:13. Kanaani, mwanawe Hamu, alilaaniwa, Mwa. 9:18–25. Utawala wa Hamu ulikuwa wa kipatriaki nao ulibarikiwa kwa vitu vya dunia na hekima lakini siyo kwa ukuhani, Ibr. 1:21–27. Mke wa Hamu, Egipto, alikuwa wa uzao wa Kaini, wana wa binti yao Egipto waliishi katika Misri, Ibr. 1:23, 25 (Zab. 105:23; 106:21–22).