Gethsemani
Bustani inayosemwa katika Agano Jipya kama iko karibu na Mlima wa Mizeituni. Katika Kiaramaiki, neno gethsemani maana yake “kinu cha kukamulia zeituni.” Yesu alikwenda katika bustani hii usiku ule ambao Yuda alimsaliti. Hapo alisali na kuteseka katika Gethsemani kwa ajili ya dhambi za wanadamu (Mt. 26:36, 39; Mk. 14:32; Yn. 18:1; Alma 21:9; M&M 19:15–19).