Misaada ya Kujifunza
Yaromu


Yaromu

Katika Kitabu cha Mormoni, ni mwana wa Enoshi na kijukuu cha Lehi. Alitunza kumbukumbu ya Wanefi kwa miaka sitini, 420–361 K.K. (Eno. 1:25; Yar. 1:13). Alikuwa mtu mwaminifu aliyechagua kutokuandika mengi katika kumbukumbu hiyo ya kihistoria (Yar. 1:2).

Kitabu cha Yaromu

Kuna aya kumi na tano tu katika kitabu hiki, katika Kitabu cha Mormoni. Yaromu aliandika kuwa Wanefi waliendelea kuishi kwa torati ya Musa na walitazamia ujio wa Kristo. Waliongozwa na wafalme waliokuwa watu wenye imani kubwa. Walisitawi walipokuwa wakiwatii manabii wao, makuhani, na walimu.