Haki ya Kuzaliwa Ona pia Agano; Mzaliwa wa Kwanza Haki ya urithi ni mali ya mzaliwa wa kwanza wa kiume. Kwa maana pana, haki ya uzawa ni pamoja na chochote au haki zote au urithi unahamishiwa kwa mtu anapozaliwa katika familia na jamii. Niuzie leo hii haki yako ya uzaliwa wa kwanza, Mwa. 25:29–34 (Mwa. 27:36). Mzaliwa wa kwanza alikaa kulingana na haki yake ya uzaliwa wa kwanza, Mwa. 43:33. Akamweka Efraimu mbele ya Manase, Mwa. 48:14–20 (Yer. 31:9). Haki ile ya uzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yusufu, 1 Nya. 5:2. Esau aliiuza haki yake ya uzaliwa wa kwanza, Ebr. 12:16. Ninyi ni warithi kisheria, M&M 86:9. Sayuni anayo haki ya ukuhani kwa njia ya nasaba, M&M 113:8 (Ibr. 2:9–11).