Nafasi ya mamlaka au wajibu katika shirika, mara kwa mara hutumika katika maandiko ili kumaanisha nafasi ya mamlaka ya ukuhani; yaweza pia kumaanisha kazi zilizopangwa katika nafasi au kwa mtu anayeshikilia nafasi hiyo.
Tulizitukuza ofisi zetu kwa Bwana, Yak. (KM) 1:19 .
Melkizedeki alipokea ofisi ya ukuhani mkuu, Alma 13:18 .
Ofisi ya huduma ya malaika ni kuwaonya watu ili watubu, Moro. 7:31 .
Mtu asitawazwe katika ofisi yoyote katika Kanisa hili pasipo kura ya Kanisa hilo, M&M 20:65 .
Acheni kila mtu asimame katika ofisi yake mwenyewe, M&M 84:109 .
Kuna marais au maafisa wasimamizi, walioteuliwa kutoka miongoni mwa wale waliotawazwa kwenye ofisi hizi katika kuhani hizi mbili, M&M 107:21 .
Kazi za wale wanaoongoza juu ya ofisi za akidi za ukuhani zinaelezwa, M&M 107:85–98 .
Na kila mtu ajifunze kazi yake, na kutenda katika ofisi ambayo ameteuliwa, M&M 107:99–100 .
Ninakupeni maofisa walio wa ukuhani wangu, M&M 124:123 .