Kuwajibika, Uwajibikaji, Wajibika Ona pia Haki ya uamuzi Bwana amesema kwamba watu wote wanawajibika kwa nia zao wenyewe, mitazamo yao, tamaa zao, na matendo yao. Umri wa uwajibikaji ni umri ule ambapo watoto wanafikiriwa kuwajibika kwa ajili ya matendo yao na kuweza kutenda dhambi na kutubu. Nitamhukumu kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, Eze. 18:30. Watatoa hesabu ya kila neno lisilo maana, Mt. 12:36. Toa hesabu ya uwakili wako, Lk. 16:2. Kila mmoja wetu atatoa hesabu yake mwenyewe kwa Mungu, Rum. 14:12. Wafu watahukumiwa kulingana na matendo yao, Ufu. 20:12. Maneno, matendo na mawazo yetu yatatushtaki, Alma 12:14. Tunajiamulia sisi wenyewe kufanya mema au maovu, Alma 41:7. Mmeruhusiwa kujiamulia ninyi wenyewe, Hel. 14:29–31. Jambo hili lifundisheni—toba na ubatizo kwa wale wenye kuwajibika, Moro. 8:10. Wote lazima watubu na kubatizwa wafikiapo katika miaka ya uwajibikaji, M&M 18:42. Shetani hawezi kuwajaribu watoto wadogo, hadi waanzapo kuwajibika mbele zangu, M&M 29:46–47. Watoto wabatizwe wakiwa na miaka minane, M&M 68:27. Kila mtu atawajibika kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe katika siku ya hukumu, M&M 101:78. Imetolewa kwa wanadamu kujua mema na maovu; kwa sababu hiyo wao ni mawakala kwao wenyewe, Musa 6:56. Wanadamu wataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao wenyewe, M ya I 1:2.