Misaada ya Kujifunza
Ufalme wa Kirumi


Ufalme wa Kirumi

Milki ya Roma ya Kale. Katika zama za kitume, Milki ya Kirumi ilikuwa yenye nguvu kubwa ulimwenguni. Ulijumuisha kila kitu kilichokuwa kati ya Frati, na Danube, Rine, Atlantiki, na jangwa la Sahara. Palestina ikawa kibaraka katika mwaka 63 K.K., wakati Pompei alipoitwaa Yerusalemu. Ingawa Warumi waliwapa Wayahudi upendeleo mwingi, Wayahudi waliuchukia utawala wa Kirumi na daima walikuwa katika uasi.

Paulo, raia wa Kirumi, alitumia Kiyunani, lugha iliyokuwa ikitumika zaidi katika ufalme huo, ili kueneza injili katika ufalme wote.