Wajibu Ona pia Mtiifu, Tii, Utii Katika maandiko, ni kazi ya kufanya, kazi iliyopangwa, au jukumu mara nyingi hutolewa na Bwana au na watumishi Wake. Uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo wajibu wa mwanadamu, Mh. 12:13. Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, Mika 6:8. Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu, Mdo. 5:29. Walipigwa kwa mateso ili kuwashtua katika kumbukumbu ya wajibu wao, Mos. 1:17. Wajibu wa wazee, makuhani, walimu, na mashemasi umeelezwa, M&M 20:38–67. Wenye ukuhani watashughulika na kazi zote za familia, M&M 20:47, 51. Wajibu wa wanachama baada ya ubatizo waelezwa, M&M 20:68–69. Wazee wangu yawapasa kusubiri kwa muda mfupi ili watu wangu wapate kujua kiukamilifu zaidi juu ya wajibu wao, M&M 105:9–10. Kila mtu na ajifunze wajibu wake, M&M 107:99–100.