Matumaini Ona pia Amini, Imani; Tegemea Kuwa na uhakikisho, kuwa na imani, kuamini katika, au imani katika jambo fulani, hususani Mungu na Yesu Kristo. Ni heri kuamini katika Bwana kuliko kumtumainia mwanadamu, Zab. 118:8. Bwana atakuwa tumaini lako, Mit. 3:26. Atapoonekana Kristo, tupate kuwa na tumaini, 1 Yoh. 2:28. Wanefi waovu wamepoteza matumaini ya watoto wao, Yak. (KM) 2:35. Ndipo tumaini lako litakapokuwa mbele ya Mungu, M&M 121:45.