Gharika katika Wakati wa Nuhu Ona pia Nuhu, Patriaki wa Biblia; Safina; Upinde wa mvua Katika wakati wa Nuhu dunia ilifunikwa kabisa na maji. Huu ndiyo ulikuwa ubatizo wa dunia na ilikuwa ishara ya kuoshwa (1 Pet. 3:20–21). Mungu ataleta gharika ya maji juu ya dunia ili kuharibu vyote vyenye mwili, Mwa. 6:17 (Musa 7:34, 43, 50–52; 8:17, 30). Maji ya gharika yakawa juu ya dunia, Mwa. 7:10. Mungu akaweka upinde katika mawingu kama ishara ya agano, Mwa. 9:9–17. Baada ya maji kupungua, nchi ya Marekani ikawa nchi teule, Eth. 13:2. Waovu wataangamia katika gharika, Musa 7:38; 8:24.