Nyumbani Ona pia Familia Nyumbani panapaswa kuwa ndiyo kituo cha injili na shughuli za kifamilia. Mwanaume atakuwa huru nyumbani mwake ili amfurahishe mke wake, Kum. 24:5. Alimtuma nyumbani kwake, Mk. 8:26. Watoto na wajifunze kuonyesha heshima kwa wazazi wao nyumbani, 1 Tim. 5:4. Kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, Tit. 2:5. Nendeni nyumbani mwenu na mkayatafakari mambo haya niliyoyasema, 3 Ne. 17:2–3. Niliwasihi wapigane vita kwa ajili ya wake zao, na watoto wao, na nyumba zao, na familia zao, Morm. 2:23. Akina baba wanaamriwa kuwa na bidii na kuwa wenye kuzijali familia zao, M&M 93:43–44, 48–50.